749
SHARES
3.6k
VIEWS

Ufugaji wa Kuku Chotara – ufugaji wa kuku chotara pdf

 

Makala hi inaeleza Juu Ufugaji wa Kuku Chotara – ufugaji wa kuku chotara pdf; aina, chakula cha kuku chotara, soko lake

Kuku chotara wana faida nyingi sana katika kilimo cha biashara. Kuku chotara ni muunganiko au mchanganyiko wa aina mbili tofauti za kuku. Kuku hawa wana faida kadhaa kwako kama mjasiriamali mwenzetu:

 1. Kuku hawa wanastahimili magonjwa. Hii inakusaidia kupunguza gharama za kuwatibu.
 2. Kuku hawa wanataga mayai mengi tofauti na kuku wa kawaida wa kineyeji. Ukiwalisha vizuri wanaweza kutaga mpaka mayai 240 kwa mwaka, huu ukiwa ni wastani wa karibia yai 1 kwa siku.
 3. Kuku hawa hukua kwa haraka na wana uwezo wa kufikia uzito wa kilogramu 3 katika muda wa miezi 3.
 4. Unaweza kuwatumia hawa kuku kwa ajili ya kuuza kama nyama au kwa ajili ya kuzalisha mayai ya biashara.

Unataka Kuwafuga Kuku Hawa Kibiashara?

Basi zingatia mambo makuu mawili:

 • Usiwaache kuku wako kuatamia mayai. Kufanya hivi unawapotezea kuku wako muda wa kutaga. Kusanya mayai yako yatie kwenye mashine ya kutotorea vifaranga. Au peleka kwa mfugaji mwenzako mwenye mashine (ambako utalipia gharama za kutotoresha kwa makubaliano).
 • Tengeneza chakula cha kuku wewe mwenyewe badala ya kununua. Kumbuka biashara yenye faida inaangalia gharama za uzalishaji dhidi ya bei ya kuuzia.

Hatua Za Ufugaji Wa Kuku Chotara

Ili kufuga kuku chotara kwa ufanisi hakikisha unafanya mambo yafuatayo;

Andaa banda ambalo linafaa kwa matumizi ya ufugaji wa kuku. Ukubwa wa banda uzingatie wingi wa kuku unaohitaji kufuga. Banda lako linatakiwa liwe linapitisha hewa ya kutosha.

Tafuta kuku wa kienyeji matetea (majike) na jogoo la kisasa aina yoyote kisha wachanganye katika banda moja. Unaweza kuanza na majike 2 na jogoo 1. Hii itapelekea upate mayai chotara.

Tumia mashine ya kutotoresha mayai ili kupata vifranga chotara. Kama haitawezekana kabisa tumia basi waache kuku waatamie mayai hayo.

Baada ya wiki tatu (siku 21) vifaranga watakuwa tayari kutotolewa kwa kutumia matetea ya kuku wa kienyeji au mashine ya kutotolesha vifaranga. Kwa muda wa wiki tatu hadi nne vifaranga wako wanahitaji joto la kutosha kwa ajili ya ukuaji na afya njema hivyo hakikisha unatumia kinengunengu kuwatunza (soma makala juu ya kinengungu hapo juu).

Vifaranga Wakiwa Tayari Chanjo Muhimu Inahitajika Ili Kuzuia Vifo Na Milipuko Ya Magonjwa Mbalimbali.

Fuata hatua zifuatazo kuhakikisha vifaranga wako wanakua vyema:

 1. Siku ya kwanza hadi ya tatu tangu kutotolewa wapatie vifaranga glukosi na vitamini pamoja na chanjo za magonjwa ya Mahepe (Mareks disease) na Mdondo (Newcastle disease).
 2. Siku ya 10 wapatie chanjo ya ugonjwa wa Gumboro.
 3. Siku ya 18 wapatie tena chanjo ya ugonwja wa Gumboro.
 4. Siku ya 21 wapatie tena chanjo ya ugonjwa wa Mdondo. Wapatie pia chanjo ya ugonjwa wa ndui (fowl pox).
 5. Wiki ya 12 (siku ya 84) wapatie kuku wako chanjo ya ugonjwa wa homa ya matumbo (fowl typhoid).

ANGALIZO:

 • Usichanganye maji ya chanjo na vitamini au glukosi.
 • Chanjo ifanyike wakati wa jioni au asubuhi. Kamwe chanjo isifanyike wakati wa mchana.
 • Hakikisha huchanji kuku wagonjwa bali wenye afya.
 • Ukishachanganya chanjo kwenye maji, kuku wanywe maji hayo kwa muda wa masaa mawili tu baada ya hapo mwaga mchanganyiko huo na osha vyombo vya maji na uweke maji safi yaliyochanganywa na vitamini.
 • Tumia vyombo vya plastiki wakati wa kuchanganya na kuwapa kuku maji ya chanjo
 • Wanyime kuku maji kwa masaa mawili kabla ya kuwapa maji ya chanjo.
 • Weka kumbukumbu za chanjo uliyotumia ikiwemo toleo la chanjo (batch number).
 • Vifaranga wapewe dawa ya kuzuia ugonjwa wa kuharisha damu (cocidiosis) kwa muda wa siku tatu mfululizo mara wafikishapo umri wa siku saba.
 • Vifaranga wapewe dawa ya minyoo wafikishapo umri wa miezi miwili (siku 60) na baada ya hapo wapewe dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu.

 

Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Welcome Back!

Login to your account below

Create New Account!

Fill the forms below to register

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.